Saturday, March 1, 2014

Mtoto kipenzi cha Mugabe kuolewa leo


Simba Chikore and his team arrive for his bachelor’s party held at a Harare hotel on Wednesday
 Mume mtarajiwa Bona Mugabe, Simba Chikore na wapambe wake wakiwasili ukumbini kwa ajili ya Bachelor Party ya kijana huyo Jumatano wiki hii jijini Harare.

HATIMAYE ili siku iliyokuwa ikisubiriwa na familia ya Rais Robert Mugabe imewadia, binti yao kipenzi, Bona Mugabe, leo anafunga ndoa na kijana, Simba Chikore katika makazi binafsi ya kiongozi huyo jijini Harare.

Bona na Simba wanafunga ndoa katoliki kati ya saa nane mchana hadi saa 10 jioni, na baadaye kutakuwa na sherehe KUBWA inayotarajiwa kuanza saa 12 jioni hadi saa 6 usiku.

Bona ni mtoto pekee wa kike wa Rais Mugabe, ni kipenzi cha mwanasiasa huyo na amewahi kutamka kuwa msichana huyo ni msikivu na mwaminifu sana hiyo mwanaume anatakayemuoa lazima ampende kwa dhati na isiwe kwa sababu ya mvuto alionao sasa.

Bona ni jina la mama mzazi wa Rais Mugabe.

No comments:

Post a Comment