Monday, March 17, 2014

Kampeni za Ridhiwani Kikwete jimboni Chalinze

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Kikwete akinong'onezwa jambo na Mmoja wa kinamama wa Kijiji cha Matipwili
Ridhiwani Kikwete akifurahia jambo na wanakijiji wa Matipwili.

Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM), Ridhiwani Kikwete akisalimiana na Sheikh wa Kijiji cha Mkange.
Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM), Ridhiwani Kikwete akisalimiana na rafiki yake wa kitambo.
Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Kikwete pamoja na Meneja wa Kampeni za Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Steven Kazidi wakiwa na Mama wa Mbunge wa Zamani wa Jimbo la Chalinze (aliefariki Dunia),Marehemu Said Bwanamdogo wakati walipofika kumjulia hali nyumbani kwake Kijijini Miono,Bagamoyo leo Machi 15,2014.
"Kijana wetu wewe ndie tunaekutaka,na amini utashinda kwa kishindo" ndivyo alivyosikika mama huyu akimwambia Mgombea Ubunge Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete.
Mkutano kwa siku ya leo ulimalizikia katika Kijiji cha Mbwewe,Pichani ni Mgombea Ubunge Jimbo la Chalinze akipita katikati ya vijana wa chipukizi wakati akiwasili kwenye Kijiji hicho.
Mgombea Ubunge Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete (kulia) akifurahia baada ya kupewa maneno ya kuvutia kutoka kwa vijana wa chipukizi.
Meneja wa Kampeni za Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Steven Kazidi (kushoto) akimtambulisha Ridhiwani Kikwete wakati wa mkutano wa kwanza wa kampeni uliofanyika katika kijiji cha Matipwili,Saadani Wilayani Bagamoyo Machi 14,2014.
Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM), Ridhiwani Kikwete akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Matipwili,Saadani Wilayani Bagamoyo,

Wananchi wakifatilia Hotuba ya Mgombea wao kwa Umakini mkubwa.
Kwa hisani ya blog ya AllyShams Blog

No comments:

Post a Comment