Wednesday, February 26, 2014

Pacha wanne waendelea vizuri



Baba wa watoto pacha wanne, Webson Simkanga na mkewe Aida Nakawala wakiwa wamewabeba watoto wao.

Watoto pacha wanne
Pacha wanne kutoka kulia ni Asifiwe, Daudi,Anania na Alinikumbu

Baba na Mama wanne wakifurahia misaada iliyotolewa na wasamaria wema kwa ajili ya familia yao.

WATOTO  wanne  pacha waliozaliwa usiku wa kuamkia Mwaka mpya wa 2014 katika Hospitali ya Wazazi ya META jijini Mbeya wanaendelea vizuri.
  Mama mzazi wa watot hao, Aida Nakawala (25) mkazi wa kijiji cha Chiwanda, Wilaya ya Momba, Mkoa wa Mbeya, amewashukuru wasamaria wema kwa kuendelea kutoa misaada iliyosaidia watoto hao kukua vizuri.
Baba Mzazi wa watoto hao, Webson Simkanga (28) amesema, hana uwezo kiuchumi lakini kutokana misaada mbali mbali aipatayo kutoka kwa wasamaria wema afya ya watoto wake inaimarika.
  Simkanga ametoa majina kwa watoto hao wanaotarajiwa kubatizwa Machi tisa mwaka huu katika kanisa la African Mission Church (AMC).
Aliwataja majina watoto hao kuanzia wa kwanza hadi wa Mwisho kuwa ni Alinikumbu (mtoto  mwenye huruma), Daudi, Asifiwe na Anania.
 
Kwa hisani ya Blog ya Mbeyayetu.

No comments:

Post a Comment