Wednesday, February 26, 2014

Bachelor party ya mkwe wa Mugabe


http://www.herald.co.zw/wp-content/uploads/2014/02/Loc13.jpg
Bwana harusi mtarajiwa, Simba Chikore na familia yake wakiwasili kwa ajili ya sherehe hiyo.

Mkwe mtarajiwa wa Rais Robert Mugabe, Simba Chikore leo anafanya sherehe ya kuagwa 'Bachelors Party' katika ukumbi wa Jacaranda uliopo kwenye jengo liitwalo Rainbow Towers jijini Harare nchini Zimbabwe.


Kwa mujibu wa kadi kwa waalikwa, sherehe hiyo itaanza saa 12 jioni leo Jumatano, na hakuna ruhusa kupiga picha wakati wa 'mnuso' huo


Inakadiriwa kuwa wageni wa kimataifa 72 wamealikwa kwenye sherehe hiyo inayotarajiwa kufanyika kukiwa na ulinzi mkali.


Simba ni rubani katika Shirika la Ndege la Qatar Airways, anamuoa binti wa Mugabe, Bona (24)Machi Mosi mwaka huu nyumbani wa kiongozi huyo.

No comments:

Post a Comment