Mshambuliaji nyota wa
zamani wa timu ya soka ya Simba na Taifa, Joseph Kaniki ‘Golota’ na
bondia Mkwanda Matumla wanashikiliwa huku Addis Ababa, Ethiopia
wakituhumiwa kusafirisha dawa za kulevya.
Kukamatwa kwao kumezidi kuongeza idadi ya Watanzania maarufu waliotiwa mbaroni nje ya nchi katika siku za karibuni wakituhimiwa kwa makosa hayo.
Kaniki na Matumla walikamatwa Agosti 31, mwaka huu kwenye Uwanja wa Ndege wa Bole, Addis Ababa wakati wakijiandaa kupanda ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia tayari kwa safari ya kuelekea Paris, Ufaransa.
Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia, Samuel Shelukindo alithibitisha jana kwamba wanamichezo hao wanashikiliwa nchini humo na Polisi wa Kitengo cha Uchunguzi wa Makosa ya Jinai.
Wanamichezo hao wamepandishwa kizimbani katika Mahakamu Kuu ya Ethiopia iliyoko kwenye eneo la

Arada, Addis
Ababa kujibu tuhuma za kubeba kilo saba za dawa hizo haramu. Mkwanda
anadaiwa kubeba kilo nne wakati Kaniki akidaiwa kubeba kilo tatu. Kama
watapatikana na hatia, wanaweza kufungwa kifungo cha miaka tisa hadi 15.
Alisema uwezekano wa kesi ya Kaniki na Matumla kurudishwa Tanzania haupo kwa kuwa nchi hizi mbili hazina utaratibu wa kubadilishana wafungwa.
“Wameshikiliwa hapa Ethiopia kwa zaidi ya siku 10 sasa, sisi tulipigiwa simu na polisi wa hapa Alhamisi iliyopita kujulishwa kwamba kuna Watanzania wawili wameshikiliwa kwa tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya, tulipokwenda tukamkuta ni Kaniki na Matumla,” alisema Shelukindo.
“Wao wenyewe wanaeleza kwamba walipitia Mombasa na huo mzigo walipewa na mtu mmoja. Lakini Kaniki yeye anajitetea kwamba huyo aliyewapa huo mzigo pale Mombasa anajuana vizuri na Mkwanda.

“Kwa hiyo alichofanya yeye ni
kuubeba tu. Walikuwa wapitie hapa Addis wakashuke Paris, Ufaransa ndipo
warudi Sweden kwa njia zao wanazojua wenyewe. Walipofika hapa Mkwanda
alifanikiwa kupenya akapanda ndege lakini Kaniki akanaswa na mbwa ndipo
akajitetea kwa polisi kwamba lile begi lilikuwa lake lakini mizigo
mingine ilikuwa ya Mkwanda.
“Ndipo hapo sasa Mkwanda akashushwa kwenye ndege wakashikiliwa na Jumatatu ya wiki iliyopita wakapandishwa kwenye Mahakama ya hapa kutajiwa kesi yao lakini hawakupewa nafasi ya kujitetea. Kesi itatajwa tena Jumanne (leo) na Jumatano (kesho) na uchunguzi wa polisi bado unaendelea.”
Wanamichezo hao walidai kwamba walikabidhiwa mizigo hiyo kwenye Uwanja wa Ndege wa Mombasa walipokuwa wakikabidhiwa pasi za kupandia ndege baada ya kupita sehemu zote za ukaguzi.
“Kilichotokea ni jambo la aibu kwa nchi na hata wachezaji wenyewe wanajuta. Kwa mfano, Kaniki anasema alikuwa aende England kucheza mpira Desemba lakini sisi tukamwambia hatuwezi kumsaidia inabidi akabiliane na kesi iliyoko mbele yake. Mkwanda yeye ametuambia kwamba anaishi Sweden hatuna maelezo yake zaidi,” alisema Shelukindo na kuongeza kuwa wamewapelekea wanamichezo hao msaada wa mablanketi kwa vile bado wako mahabusu na Ethiopia kwa sasa kuna baridi kali.

Wavuti.com
No comments:
Post a Comment