Thursday, August 1, 2013

Wamiliki wa mitandao waonywa


 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Profesa John Nkoma akizungumza na wadau mbali mbali wa maswala ya habari nchini wakiwemo wamililiki wa magazeti tando (Bloggers) kuhusu kampeni mpya ya kuhamasisha matumizi mazuri ya Mitandao ya Mawasiliano hapa nchini ,iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Sinza B,jijini Dar es Salaam.
Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Innocent Mungy akifafanua jambo wakati wa Warsha ya siku moja kwa wadau mbali mbali wa maswala ya habari hapa nchini wakiwemo wamililiki wa magazeti tando (Bloggers) kuhusu kampeni mpya ya kuhamasisha matumizi mazuri ya Mitandao ya Mawasiliano ,iliyofanyika  kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania,Uliopo eneo la Sinza B,jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Profesa John Nkoma akibonyeza kitufe kwenye Kompyuta ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa Wimbo wa kampeni mpya ya kuhamasisha matumizi mazuri ya Mitandao ya Mawasiliano nchini.
Sehemu ya Washiriki wa Warsha kwa wadau mbali mbali wa maswala ya habari hapa nchini wakiwemo wamililiki wa magazeti tando (Bloggers) kuhusu kampeni mpya ya kuhamasisha matumizi mazuri ya Mitandao ya Mawasiliano ,iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Sinza B,jijini Dar es Salaam.
Msanii wa Muziki wa Kiasili, Mrisho Mpoto akisisitiza jambo kuhusu umuhimu wa Mawasiliano Mazuri ya Mitandao wakati wa Warsha ya siku moja kwa wadau mbali mbali wa maswala ya habari nchini wakiwemo wamililiki wa magazeti tando (Bloggers) juu ya kampeni mpya ya kuhamasisha matumizi mazuri ya Mitandao ya Mawasiliano ,iliyofanyika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Sinza B,jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa Wamiliki wa Magazeti tando nchini (Blogger), John Bukuku kutoka Full Shangwe Blog akitoa shukrani zake za dhati kwa TCRA ikiwa ni kwa niaba ya Bloggers Wengine baada ya kutambuliwa kuwa ni sehemu ya Vyombo ya Habari nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Profesa John Nkoma (katikati) akiwa na baadhi ya wamiliki wa mitandao ya kijamii (Bloggers),wa tatu kushoto ni Meneja Mawasiliano wa Mamlaka hiyo, Innocent Mungy.

MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeonya wamiliki wa mitandao ya mawasiliano ya kijamii ikiwemo blogu, wanaoitumia vibaya na kuhatarisha amani kwa kusambaza ujumbe za chuki.


Imetaka waache mara moja kabla hatua kali za kisheria hazijachukuliwa dhidi yao. 


Mkurugenzi Mtendaji wa TCRA, Profesa John Nkoma aliyasema hayo jana, Dar es Salaam wakati wa warsha ya uzinduzi wa kampeni ya “Futa Delete Kabisa” ya kuhamasisha matumizi mazuri ya mitandao ya mawasiliano. 


Akizungumza katika warsha hiyo iliyoshirikisha wamiliki wa blogu na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini, kabla ya kuzindua wimbo maalumu wa kampeni hiyo, Profesa  Nkoma alisema kampeni hiyo itakayofanyika kupitia vyombo vya habari,  inalenga kuimarisha amani ya nchi.


“Tanzania tumekuwa na amani lakini sasa hivi tunaichezea, ujumbe mkubwa tulionao kama mamlaka ni kwamba, tusifanye mchezo, TCRA inatambua umuhimu wa mitandao ya mawasiliano, ni kitu kizuri na tunajivunia ukuaji wake, lakini tusipoitumia vizuri, tutakuja juta,” alisema Prof. Nkoma na kuongeza.


“Matumizi ya blogu kupitia intaneti nchini ni ya kujivunia lakini yakitumika kuchukiana, nchi ikaharibika, hatuna pa kukimbilia, tusizitumie kueneza chuki za kidini, siasa na ukabila, tunatambua wapo wanaotumia vibaya mitandao kutaka kuvuruga amani, matusi mtandaoni hayatusaidii, ukipata ujumbe mbaya, ufute na si kuusambaza”.


Prof Nkoma alisema ingawa TCRA haihusiki kutoa leseni kwa wamiliki wa blogu nchini, lakini kwa kuwa ni mdhibiti wa mawasiliano na wanatambua mitandao hiyo kama sehemu ya vyombo vya kupasha habari jamii, ni vyema wamiliki wakaheshimu sheria za nchi za mawasiliano.


Meneja Mawasiliano wa TCRA, Innocent Mungy alisema mamlaka hiyo itakaa na wamiliki wa blogu wafahamu nguvu ya habari wanazoandika, wajifunze habari ni nini ili wajiepushe na uchochezi. Aliwataka waandike matukio ya mijadala ya kujenga taifa na si fulani kala nini.


Chanzo picha: Habarileo, Picha- Habarimseto Blog

No comments:

Post a Comment