
Askofu Mkuu wa kanisa la Evangelistic Assemblies God Tanzania, Moses Kulola amefariki dunia leo jijini Dar es Salaam.

ASKOFU
MOSES KULOLA (katikati) AKIWA NA WAIMBAJI WA MUZIKI WA INJILI FAUSTINE MUNISHI NA
EMMANUEL MWASOTA NA HAPA ILIKUWA NI MWANZONI MWA MIAKA YA 1970.Askofu Kulola, ambaye amezaliwa mwaka 1928, amekuwa akisumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu na kuna wakati alipelekwa India kwa matibabu.
Mmoja wa watu wa karibu wa familia ya Askofu huyo amesema, kiongozi huyo wa Kanisa alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya moyo, mapafu na ini.
Askofu Moses Kulola akiwa Israel




No comments:
Post a Comment