Wednesday, July 24, 2013

Askari aliyeuawa Darfur alivyozikwa Songea

 Askari wa JWTZ wakiwa wamebeba mwili wa Rodney Ndunguru
Aliyekaa katikati mbele ni mama mzazi wa Rodney Ndunguru
 
 Umati wa watu uliojitokeza katika mazishi ya Rodney Ndunguru katika makaburi ya  mjimwema
 Mwili wa Rodney Ndunguru ukiingizwa kaburini
 Mama wa marehemu Rodney Ndunguru akiweka shada la maua katika kaburi la mwanawe
---------------------------------------
Na Cresensia Kapinga,Songea.


SIMANZI ,Vilio,majonzi  vimetawala wakati wa mazishi na maziko ya askari wa Jeshi la Wananchi Rodney Ndunguru wa kikosi cha makomando cha 92 KJ Ngerengere mkoani Morogoro.
 
Mamia ya wakazi wa Mkoa wa Ruvuma wakiwemo askari wa Jeshi la wananchi walihudhuria mazishi yaliyofanyika jana kwenye makaburi ya Mjimwema Manispaa ya Songea.

  Maziko hayo yaliongozwa na Paroko wa kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Songea Parokia ya Mjimwema Padre Noel Duwe.
 
Padre Duwe aliwaonya Watanzania wasichezee amani  na kwamba, utulivu uliopo  ulindwe kwa namna yoyote.

Picha zote kwa hisani ya blog ya Songea Yetu

No comments:

Post a Comment