Thursday, July 18, 2013

Anaomba 400,000/- afanyiwe upasuaji wa nyonga




JAMES Lutwe (43) mkazi wa Bunju 'B' katika Manispaa ya Kinondoni Dar es Salaam anaomba msaada wa Sh 400,000 ili afanyiwe upasuaji wa nyonga iliyovunjika baada ya kuangukiwa na kifusi.

Akizungumza na gazeti hili Dar es Salaam jana, mkazi huyo ambaye kwa sasa anatembelea magongo, alisema alitakiwa kufanyiwa operesheni tangu Julai mwaka jana alipopata ajali, lakini ilishindikana kutokana na kukosa fedha.

Kwa mujibu wake, matibabu yote yanagharimu Sh milioni 10.3 lakini kutokana na ukweli alioueleza kuwa hana ndugu au jamaa mwenye uwezo wa kuzilipa, madaktari wanaomshughulikia katika Taasisi ya Mifupa (MOI) walimwelewa na wametafuta namna ya kumsaidia hivyo kaambiwa atafute Sh 400,000.

"Naomba msaada kutoka kwa yeyote atakayeguswa na tatizo langu kwa sababu ninapata maumivu makali na hakuna kazi ninayoweza kuifanya kwa sasa. 

Fedha zitanifikia zikitumwa kupitia namba hizi za simu; 0762879490 na 0656214438".

Lutwe alipata ajali hiyo katika eneo la Mto Mpiji alipokuwa akijaza mchanga wa kuuza kwenye malori.

Chanzo: HabariLEO

No comments:

Post a Comment