Kuna taarifa zinazodai kuwa, msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini, Langa Kileo amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam.
Akiwa kidato cha pili alihamishiwa Kampala, Uganda katika Shule ya Vienna na baadaye Shule ya Hillside International Academy, huko huko Uganda.
Buriani Langa.
Langa alishiriki shindano la Pop Star akiwa na
wenzake wengine wawili Sara Kaisi 'Shaa' na Witness Mwaijaga 'Witness' na
waliunda kundi lilioenda kwa jina la Wakilisha.
Wakiwa na kundi la Wakilisha Marehemu langa na
Wenzake hao walitamba sana kwa nyimbio mbili za 'Unaniacha Hoi' na
'Kiswanglish'.
Langa aliamua kutoka kivyake na kuachia kibao chake
cha kwanza cha 'Matawi ya Juu' na video ya wimbo huo ikaingizwa katika
mashindano ya MTV Base na baade kushinda tuzo ya Kisima nchini Kenya.
Aliwahi fanya kazi na wasanii mbalimbali wa nchini
na nje ya nchi kama vile kundi la Necessary Noise,
Naaziz na Wyre (Kevin Wyre).
Maisha ya Langa
kimuziki yalianza kuporomoka pale alipoachia albam yake ya 'Langa' na kushindwa
kuuza baada ya kukataliwa na wasambazaji na akaamua kutumia dawa za kulevya.
Baada ya jitihada za
familia yake aliweza kuondoka katika maisha hayo ya uteja na alipo toka
aliachia nyimbo za 'Bombokiata' na 'Mteja Aliyepata Nafuu'.
Langa alizaliwa mwaka 1985 jijini Dar es Salaam akiwa tunda la wanandoa Vanessa Kimei na mumewe
Mengisen Kileo.
Alipata elimu ya
msingi katika shule ya Msingi Olympio na baade Sekondari ya Loyola, zote za jijini Dar es
Salaam.
Akiwa kidato cha pili alihamishiwa Kampala, Uganda katika Shule ya Vienna na baadaye Shule ya Hillside International Academy, huko huko Uganda.
Baadaye
alirejea nchini na kujiunga na masomo ya Stashahada ya Masoko katika Chuo cha
Biashara Dar es Salaam (CBE), Kampasi ya Dodoma.
DUUUUUUUUH EBWANA EEEEEEEEEEEE KUMBE JAMAA ALISHAWAHI KUWA TEJA !
ReplyDelete