WANAFUNZI wa kike wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM),
Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) na Chuo cha Mamlaka ya Elimu na Ufundi Stadi
(VETA), Dar es Salaam, wamefikishwa katika Mahakama ya Jiji Samora, wakidaiwa
kufanya biashara ya kuuza miili yao.
Washtakiwa hao walikamatwa katika eneo la Kona Baa
Ambiance, Sinza wilayani Kinondoni ambao ni miongoni mwa wanawake 35 wanaodaiwa
kufanya biashara hiyo na wote walifikishwa mahakamani hapo.
Kesi hiyo ilikuwa chini ya Hakimu Willian Mtaki ambapo
Mwendesha Mashtaka,
. John Kijumbe, alisema wasichana hao walikamatwa katika
mazingira tofauti tofauti.
Wanafunzi hao ni Yasinta Kilimo mwenye miaka 21 (CBE),
mkazi wa Upanga, Morin Masatu miaka 19 (UDSM), mkazi wa Kinondoni na mwanafunzi
wa VETA, aliyefahamika kwa jina moja la Khadija.
“Nilikwenda
pale baa kuchukua simu yangu ambayo ilipotea hivyo waliniita nikaichukue ndipo
askari wa jiji wakanikamata,” alisema Khadija wakati akijitetea.
Kwa mujibu wa
Bw. Kijumbe, washtakiwa hao wamekosa dhamana baada ya kushindwa kutimiza
masharti ya kila mmoja kuwa na wadhamini wawili au kulipa faini sh. 200,000.
Kesi hiyo
inatarajiwa kusikilizwa tena Mei 28 mwaka huu, ambapo washtakiwa wote
walipelekwa Segerea.
No comments:
Post a Comment