Rais
Jakaya Kikwete na mkewe mama Salma Kikwete wakipokea maua mara
baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta
jijini Nairobi kuhudhuria kuapishwa kwa Rais wa Nne wa
Kenya Uhuru Kenyatta katika Uwanja wa Kasarani leo.
Maelfu ya wananchi wa Kenya tayari wamejaa uwanjani kusubiri kushuhudia tukio hilo la kihistoria.
Rais
Jakaya Kikwete na mkewe mama Salma Kikwete na Balozi wa Tanzania
nchini Kenya Dkt Batilda Burian wakipozi na wasichana waliowazawadia
mashada ya maua mara baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Kimataifa
wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi kuhudhuria sherehe za kuapishwa
kwa Rais wa Nne wa Kenya Uhuru Kenyatta.
Rais
Jakaya Kikwete na mkewe mama Salma Kikwete wakilakiwa kwa
heshima zote baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo
Kenyatta jijini Nairobi tayari kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais
wa Nne wa Kenya Uhuru Kenyatta na Makamu wake, William
Ruto katika uwanja wa michezo wa Kasarani April 9, 2013
No comments:
Post a Comment