Friday, March 29, 2013

Jengo la ghorofa 16 laporomoka Dar es Salaam

 Nondo nyembamba zilizokuwa zikitumika kujenga jengo hilo zimeacha maswali mengi yasiyo na majibu
 Askari wakiimarisha ulinzi wakati kazi ya uokoaji ikiendelea.
 Jitihada za kuwaokoa watu zikiendelea.
Waokoaji.


 Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam (CP), Suleima Kova kuhusu jengo la ghorofa 16 lililoanguka leo saa mbili asubuhi katika makutano ya mtaa wa Indira Ghandi na Barabara ya Morogoro jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi.

 Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleima Kova akizungumza na waandishi wa habari kwenye eneo la tukio.
 Kamanda wa Polisi Kanda Maalum (CP), Suleima Kova akiwa katika eneo la tukio. Kulia ni Mbunge wa Kuteuliwa, James Mbatia.
 
Picha zote kwa hisani ya Blog ya Habari Mseto

1 comment:

  1. NIMESIKITIKA SANA KUPATA HABARI HII, KWANI WATANZANIA WASIOKUWA NA HATIA WANAANGAMIA, KITU CHA MSINGI TUNAIOMBA SERIKALI IONGEZE KIKOSI CHA UOKOAJI ILI KUNUSURU MAISHA YA WALE AMBAO KWA UWEZO WA MUNGU YAWEZEKANA WAKAWA HAI, VILE VILE WATANZANIA SIO MDA WAKUANZA KULAUMIANA KWA WAKATI HUU CHA MSINGI TUUNGANE KWA WAKATI HUU MGUMU,VILEVILE TUWATIE MOYO WALE WANAOHUSIKA ZAIDI NA JANGA HILI KUBWA HAPA TANZANIA

    ReplyDelete