Tuesday, February 12, 2013

CCM yatangaza wajumbe wa Kamati Kuu

Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi katika kikao chake cha siku mbili Februari 10 na 11, 2013 kilichofanyika mjini Dodoma, pamoja na mambo mengine kimeridhia uteuzi na kufanya uchaguzi wa Wajumbe 14 wa Kamati Kuu yake.

Wajumbe wa NEC wakiwa tayari kupiga kura




Makatibu wa NEC,Kutoka kushoto Zakia Meghji, Dk. Asha-Rose Migiro na  Mohamed Seif Khatib



Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal akipiga kura kuchagua wajumbe wa Kamati Kuu ya  CCM

Makamu wa pili wa Rais Zanzibar , Balozi Seif  Ali Idd na Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Mwigulu Nchemba wakipiga kura kuchagua wajumbe wa kamati kuu ya CCM,Taifa.   


(Baadhi ya picha kwa hisani ya blog ya CCM)
 
Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM imeridhia uteuzi wa Dokta Salim Ahmed Salim kuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu kupitia nafasi 10 za uteuzi wa Mwenyekiti wa CCM.  Wajumbe 14 waliochaguliwa kuwa wajumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ni:- 
Wajumbe wa Kamati Kuu - Bara

1. Ndugu Pindi Chana
2. Ndugu Adam Kimbisa
3. Ndugu William Lukuvi
4. Dokta Emmanuel Nchimbi
5. Ndugu Jerry Silaa
6. Profesa Anna Tibaijuka
7. Ndugu Stephen Wassira

Wajumbe wa Kamati Kuu - Zanzibar

1. Ndugu Shamsi Vuai Nahodha
2. Ndugu Hussein Mwinyi
3. Profesa Makame Mbarawa Mnyaa
4. Dokta Salim Ahmed Salim
5. Ndugu Maua Daftari.
6. Ndugu Samia Suluhu Hassan
7. Ndugu Hadija H. Aboud
Imetolewa na:-       
Nape Moses Nnauye, KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA ITIKADI NA UENEZI 12/02/2013

No comments:

Post a Comment