Thursday, February 21, 2013

Buriani Padri Mushi

Padri Mushi aliuawa kwa kupigwa risasi, Jumapili iliyopita wakati akijiandaa kwenda kuongoza misa katika Kanisa la Mt. Joseph Minara Miwili mjini hapa.

Ibada ya mazishi iliyoongozwa na Askofu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo ilianza saa nne asubuhi katika Kanisa la Mt. Joseph Minara Miwili na kuhudhuriwa pia na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein.
Baada ya misa hiyo iliyomalizika saa 6.30 mchana, msafara wa waombolezaji ulikwenda  Kitope yalipo makaburi ya viongozi wa Kanisa Katoliki. 

Baada ya kufika makaburini, ibada ya mazishi ilianza saa 7.30 mchana na mwili wa Padri uliwekwa kaburini saa moja baadaye.

No comments:

Post a Comment