Friday, November 2, 2012

Wanaotuhumiwa kumuua RPC Barlow hawa hapa

  Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Said Mwema


Watu watano wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi mkoa wa Mwanza wakituhumiwa kuhusika kumuua Kamanda wa Polisi mkoa huo, Liberatus Barlow.
 
Watuhumiwa hao ni  Muganyizi Michael (36) mkazi wa Nyakabung; Magige Marwa maarufu kwa jina la “Tatoo”(48), mkazi wa Bugarika; Chacha Mwita (50) mkazi wa Gongolamboto Dar es Salaam;  Buganze, Edward Luseta (22), mkazi wa Tandika  na Bhokle Mwita (42) mkazi wa Ukonga Mombasa, Dar es Salaam.

Wanadaiwa kuhusika kumuua RPC Barlow, usiku wa Oktoba 13, mwaka huu  eneo la Minazi Mitatu Kitangiri wilaya ya Ilemela.

Watuhumiwa wengine watano akiwemo Mwalimu Doroth Moses Lyimo aliyekuwa na Kamanda Barlow wakati tukio  hawakufikishwa mahakamani.

Watu wengine waliokuwa wakishikiliwa na kuhojiwa kuhusiana na mauaji ya Barlow, lakini hawakufikishwa mahakamani ni Felix Felician (50), Philemon Felician maarufu kama “Fumo” (46) aliyewahi kuzichezea klabu za Pamba ya Mwanza na Yanga ya Dar es Salaam ambaye pia ni mdogo wa Felix, Bahati Lazaro (28) na Amos Woibe Mabhoto maarufu kama “Bonge” (30), wote wakazi wa jijini Mwanza.

No comments:

Post a Comment