Sunday, November 25, 2012

Wanafunzi UDOM wadaiwa kujiuza


  Wanafunzi wa kike katika chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) wanadaiwa kufanya biashara ya ukahaba katika maeneo mbalimbali ya starehe mjini Dodoma!

Inadaiwa kuwa wasichana hao wanauza miili yao kwa lengo la kujikimu kimaisha.

Tuhuma hizo zimebainika wakati wa mahafali ya tatu ya UDOM huku takribani wahitimu 6392 wakitunukiwa vyeti, stashahada, Shahada za kwanza, shahada za uzamili na shahada za Uzamivu.

Kuna madai kwamba, wanafunzi hao huondoka chuoni usiku na kujiunga na  wasichana wa mitaani waliokubuhu kwenye ukahaba maarufu kama machangudoa.
Wakizungumza na star tv wakati wa mahafali ya UDOM , baadhi ya wahitimu wamethibitisha uwepo wa vitendo hivyo vilivyo kinyume na maadili. 
Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof.Idris Kikula ametoa onyo kali kwa wote watakaobainika. 

No comments:

Post a Comment