Tuesday, October 16, 2012

Warioba- Tunakusanya maoni, si wakati wa kura


Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba (kulia) akizungumza na wajumbe wa kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala wakati wa ziara iliyoanywa na wajumbe hao leo jumanne tarehe 16.Oktoba, 2012  ya kutembelea vitengo mbalimbali vilivyopo katika Makao Makuu ya Tume hiyo Jijiini Dar es Salaam. 
 
Kushoto ni Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Angellah Kairuki na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Pindi Chana. (Picha na Tume ya Katiba)


Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, (kulia) akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala, Pindi Chana (katikati) wakati kamati hiyo iliyofanywa leo jumanne tarehe 16. Oktoba, 2012 na kutembelea vitengo mbalimbali vilivyopo katika  makao makuu ya Tume hiyo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Angellah Kairuki. (Picha na Tume ya Katiba)


Katibu wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba akibadilishana mawazo na wajumbe wa kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala wakati wa ziara ya wajumbe hao iliyofanywa leo jumanne tarehe 16.Oktoba, 2012 na kutembela vitengo mbalimbali vilivyopo katika Makao Makuu ya Tume hiyo, Jijini Dar es Salaam. Kutoka Kulia ni wajumbe wa Kamati hiyo, Rashid Ali Abdalla, Deogratius Ntukamazina, Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Angellah Kairuki na Felix Mkosamali. (Picha na Tume ya Katiba)


Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala wakitazama namna ya Sauti zenye maoni ya wananchi zinazokusanywa kutoka Mikoa mbalimbali nchini namna zinavyoweza kupokelewa katika Makao makuu ya Tume hiyo, Jijini Dar es Salaam.  (Picha na Tume ya Katiba)
======================================================================
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba amesisitiza umumihu wa wananchi kutoa maoni maoni yao kuhusu Katiba Mpya badala ya kukimbilia kuwasilisha maoni waliyolishwa na viongozi wa vyama vya siasa, asasi za kiraia na kidini.

Jaji Warioba ameyasema hayo leo katika mkutano kati ya Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala na uongozi wa Tume hiyo uliofanyika katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Warioba, baadhi ya viongozi na wadau wengine wanadhani uamuzi wa kazi ya kukusanya maoni inayofanywa kwa sasa na Tume utaauliwa kwa kura na hivyo kuwalisha wananchi maoni ili wayatoe kwa tume kwa wingi.

“Wengine wanafikiri huu ni wakati wa kupiga kura…hapana, sisi tunatafuta hoja,” alisema Mwenyekiti huyo na kuwataka wadau mbalimbali kuwaacha wananchi watoe maoni yao binafsi.

No comments:

Post a Comment