Tuesday, October 23, 2012

Vijana CCM kupambana Dodoma



Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) umetamba kuwa utahakikisha kuwa vitendo vya rushwa havitokei katika uchaguzi mkuu utakaofanyika kuanzia leo katika ukumbi wa Mwl. Nyerere katika Chuo Cha Mipango mjini Dodoma.

UVCCM imeonya kuwa, mgombea au hata mpambe atakayebainika kujihusisha na kampeni zilizo nje ya utaratibu na kanuni za UVCCM au kujihusisha na vitendo vya rushwa atashughulikiwa mara moja.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM, Martine Shigela akizungumza
na waandishi wa habari  jana mjini Dodoma.
 Katibu Mkuu wa umoja huo, Martine Shigela, jana aliwaambia waandishi wa habari mjini humo kuwa, wameweka mtandao wa kutosha kukabiliana na aina yoyote ya ukiukwaji wa tararibu, kanuni na sheria za uchaguzi wa UVCCM.

 "Sisi hatuwezi kuzungumzia hayo mnayosema, yamejitokeza kwenye uchaguzi wa UWT, lakini kwa upande wetu tunawahakikishieni kwamba tutamkabili vilivyo tena bila mzaha, mgombea au mpambe yeyote atakayejaribu kutumia mbinu chafu za kampeni ikiwemo kutoa rushwa", alisema Shigela.

No comments:

Post a Comment