Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza. Liberatus Barlow ameuawa kwa kupigwa risasi usiku wa kuamkia leo jijini humo.
Kamanda Barlow alipigwa risasi saa 7 usiku eneo la Kitangiri wakati akitoka kumshusha dada yake.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP, Said Mwema, amesema, watu wawili walimvamia Kamanda Barlow na kumuua kwa kumpiga risasi.
Kabla ya tukio hilo, Kamanda Barlow alikuwa kwenye kikao cha harusi ya ndugu yake.
Hadi sasa chanzo cha mauaji hayo hakijafahamika.
No comments:
Post a Comment