Tuesday, October 2, 2012

Meli mpya ya Azam Marine yawasili Zanzibar



Kampuni ya Azam Marine imeleta meli mpya ya kisasa yenye uwezo wa kubeba abiria 1500 na magari 200 kwa wakati mmoja.
 
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Azam Marine, Bw. Hussein Mohammed Saidi, amesema mjini Zanzibar kuwa meli hiyo ambayo itafanya safari zake kati ya Dar es Salaam, zanzibar na Pemba itatoza nauli nafuu.
 
Amesema meli hiyo iliyotengenezwa Ugiriki inatarajiwa kuanza safari zake mara baada ya kukamilisha taratibu za mamlaka mbalimbali.
 
Meli hiyo inayoitwa AZAM SEALINKI ni ya kisasa katika ukanda huu wa Mwambao wa nchi za Kusini na Pembe ya Afrika.
 
  Wakazi wa Zanzibar wakipiga picha Meli wakati ikiwasili Zanzibar jana.
Mzee Said Bakheresa (mwenye nguo nyeusi) akikagua mazingira ya Meli hiyo baada ya kuwasili Bandari ya Zanzibar .
Sehemu ya kuegesha magari.
  Sehemu ya kupumzikia wasafiri.
(Picha na Omar Said wa Kampuni ya Bakheresa).
Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi Zanzibar
 
Saidi amesema, meli hiyo itasafiri kwa muda wa saa tatu kutoka Dar es salaam na Zanzibar na saa 4 kutoka Zanzibar na Pemba ama saa 7 kutoka dar es salaam na Pemba.
 
Amesema pamoja na kuwasili kwa Meli hiyo, Kampuni ya Azam pia inatarajia kuleta meli nyingine ya abiiria inayojulikana kama Kilimanjaro namba 4.
 

No comments:

Post a Comment