Kamanda Liberatus Barlow
TUKIO la kuuawa kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow sasa linahusishwa na kisasi cha mapenzi, imefahamika.Polisi tayari wamemkamata mtu mmoja anayedaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi Mwalimu Dorothy Moses.
Siku ya tukio, usiku wa kuamkia Jumamosi iliyopita, mwalimu huyo alikuwa na Kamanda Barlow hadi wakati RPC huyo anapigwa risasi nje ya nyumba anapoishi mama huyo anayedaiwa kuwa mjane.
Kuna taarifa zinazodai kwamba, Mkurugenzi
wa Makosa ya Jinai, DCI, Robert jana alithibitisha kukamatwa
kwa mtu huyo (jina tulihifadhi) akisema:
“Ni kweli mtu mmoja
amekamatwa, lakini kwa sasa siwezi kuzungumzia kwa kina kuhusu suala
hilo kwa sababu bado tunamhoji na tunaendelea na uchunguzi.
Tutakapokamilisha, tutatoa taarifa.”
Kaimu
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Lily Matola pia alithibitisha
kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo. Hata hivyo, alisema amesikia habari hizo
kwa kuwa yuko safarini kwenda mkoani Kilimanjaro kwenye mazishi ya
kamanda huyo...
“Hayo nimesikia, lakini kwa sasa sipo Mwanza hivyo
siwezi kuzungumzia lolote.”
Habari
za uhakika kutoka ndani ya Jeshi la Polisi, zinadai kuwa, upelelezi
wa mauaji hayo umefanikiwa kwa hatua kubwa.
Mtu huyo
alikamatwa Dar es Salaam baada ya kuwekewa mtego na makachero waliopo
katika timu ya uchunguzi na alisafirishwa hadi Mwanza ambako
anashikiliwa na jeshi hilo.
Ilielezwa kuwa mtu huyo alikamatwa kutokana na kuwapo kwa taarifa za siri za kiitelejensia kutoka kwa watu mbalimbali.
“Kuna
hali imefunguka na imesaidia sana. Inaonyesha kwamba Dorothy alikuwa
na uhusiano na mtu huyu ambaye alikuwa akifika nyumbani kwake, kama
mumewe na watu wanajua jambo hili,” alieleza mmoja wa askari polis.
Alisema
kwamba uchunguzi wa awali unaonyesha kwamba uamuzi wa mwalimu huyo
kusitisha uhusiano wa mapenzi na mtu huyo huenda ndicho chanzo cha
mauaji hayo lengo likiwa ni kumshawishi Dorothy kurejesha uhusiano.
Mwalimu Doroth Moses aliyekuwa na RPC Barlow
“Mimi
natambua kwamba huyu jamaa na Dorothy walikuwa na uhusiano na
inajulikana mjini kuwa hata mke wa mtuhumiwa anatambua jambo hilo
kwani walishagombana siku moja mjini na hata katika msiba nyumbani kwao
na mtuhumiwa,” alisema mama mmoja (jina tunalo), aliyejitambulisha
kama mmoja wa marafiki wa karibu wa Dorothy.
Mwanafunzi
wa Shule ya Sekondari Kitangiri (jina tunalo), anasema amekuwa
akimfahamu mtuhumiwa aliyekamatwa kama baba mwenye nyumba hiyo na kila
mara amekuwa akimkuta hapo nyumbani wakati wa kujisomea na wanafunzi
wenzake.
“Mimi ninamfahamu kama baba wa rafiki yangu na nimewahi kumkuta wakati wa kujisomea hapo nyumbani na watoto wa nyumba hiyo.”
Hili
ndilo geti la nyumba anayoishi Mwalimu Doroth Moses, katika eneo la Kitangiri jijini Mwanza.
Pembeni ya geti hilo ndipo alipouawa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow.
Dorothy
ambaye ametajwa kuwa mjane, ni Mwalimu katika Shule ya Msingi
Nyamagana na tangu kufariki dunia kwa mumewe Ofisa wa zamani wa TRA, Modest
Lyimo mwaka 1997.
“Watu
wote wanajua kwamba mtuhumiwa alikuwa akitembea na huyo mwalimu,
wameonekana mara nyingi wakiwa muziki,” alieleza mmoja wa ndugu wa
karibu wa mke wa mtuhumiwa.
Blog za Mikoa
No comments:
Post a Comment