Wednesday, October 10, 2012

Binti afanya mtihani wa taifa wodini

Mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya sekondari ya Alfa Morogoro, Jesca Kiliani (17) akifanya mtihani wa taifa wa kidato cha nne akiwa katika wodi namba 7B  katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Morogoro . 
 MWANAFUNZI wa kidato cha nne katika Sekondari ya Alfa Germ, Morogoro, Jessica Kiliani (17), amelazimika kufanya mtihani wake wa kuhitimu elimu ya sekondari akiwa wodini baada ya kufanyiwa upasuaji.
 
Hatua hiyo ilifikiwa baada ya mwanafunzi huyo, kuomba aruhusiwe kufanya mtihani huo licha ya kuwa  wodini akiugulia maumivu ya upasuaji aliofanyiwa na madaktari wa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro kwa zaidi saa ya mbili na kulazwa katika wodi ya wazazi namba 7B.


Mama mzazi wa mwanafunzi huyo, Anna Ngapemba alisema, alipigiwa simu na mkuu wa shule hiyo 6:00 usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili iliyopita akimjulisha kuwa binti yake anasumbuliwa na tumbo na anahitaji msaada wa haraka.


Ngapemba amesema, alilazimika kwenda shuleni hapo usiku huohuo na kukutana na mama mlezi (matron) wa hosteli za shule hiyo na kujulishwa kuhusu hali ya binti yake na kwa kushirikiana na uongozi wa shule hiyo, walimpeleka katika Hospitali ya Mkoa.


Alisema wauguzi waliokuwa zamu usiku huo walilazimika kumpigia simu daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake, Christopher Manumbu ambaye alifika na kumfanyia upasuaji.


Mama huyo alisema binti yake aliwahi kulalamika kuwa na maumivu ya tumbo wakati alipokuwa kidato cha pili mwaka 2010 lakini baada ya kupatiwa matibabu, hali hiyo haikumtokea tena hadi Jumamosi iliyopita.


Baada ya upasuaji huo, Dk Manumbu alisema binti huyo alihitaji upasuaji wa haraka ili kutokana na hali yake kuwa mbaya.


Akiwa chini ya msimamizi wa mitihani na polisi, Jessica licha ya kuwa katika hali ya maumivu alifanya mitihani miwili kama wenzake wa kidato hicho. Mitihani hiyo ni Uraia na Kiingereza.
 
Mwanafunzi huyo alisema hakuwa tayari kuikosa mitihani hiyo na ndiyo maana alimwomba mama yake kuwasiliana na uongozi wa shule yake ili umwandalie mazingira mazuri ya kufanya mtihani akiwa wodini.

 Blog za mikoa

2 comments:

  1. MUNGU akusaidie katika kile ulichopanda ukivune mtoto mzuri, hongera pia kwa ujasiri

    ReplyDelete
  2. I enjoyed reading your this informative article and considering the points you made. You make a lot of sense. This is an excellent piece of writing. Thanks for sharing this so we can all read it.

    Webzemini Software - website design Company and Software Company

    ReplyDelete