Wednesday, June 6, 2012

Lori lilivyogonga basi na kuua watu 13 Mbeya

 Wananchi wakisaidia uokoaji katika eneo la ajali 

 Picha zikionyesha ajali iliyoyahusisha basi dogo aina ya Toyota Coaster na lori la mizigo iliyotokea katika Kijiji cha Ntangano, Ijombe Mbeya Vijijini barabara ya Mbeya- Kyela.

WATU 13 wamekufa na wengine kadhaa kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha magari mawili eneo la Ntangano Ijombe Mbeya Vijijini barabara ya Mbeya Kyela.

Ajali hiyo imelihusisha lori lenye namba T.658 ASJ lililokuwa na tela namba T.150 ASN iliyokuwa ikitokea mpakani mwa Tanzania na Malawi (Kasumulo) pamoja na Toyota Coaster yenye namba T.886 BDZ iliyokuwa ikitoka Jijini Mbeya kuelekea Wilayani Kyela.



 Wananchi waliofika Hospitali ya Rufaa Mbeya kutazama miili ya marehemu
 Miili ya marehemu ikipelekwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya
 Wafanyakazi wakiwawahisha majeruhi kupata huduma ya kwanza.

Picha kwa hisani ya www.mbeyayetu.blogspot.com na www.francisdande.blogspot.com

No comments:

Post a Comment