Monday, June 4, 2012

Chadema walivyotikisa Mtwara

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasa na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa (kulia), akizungumza baada ya kufungua moja ya matawi mjini Newala ikiwa ni sehemu ya ziara ya viongozi wa chama hicho. Katikati ni Mwenyekiti, Freeman Mbowe akiwa amembeba mtoto Muaza Mohamed na kushoto ni Mkamu Mwenyekiti, Zanzibar, Ali Issa Mohamed.
 Akinamama wa kijiji cha Mbuyuni, katika jimbo la Lulindi mkoani Mtwara, wakiimba nyimbo za kumpongeza Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freema Mbowe, mara baada ya mkutano wake wa hadhara katika kijiji hicho
Akinamama wa kijiji cha Mbuyuni katika jimbo la Lulindi mkoani Mtwara, wakiitikia kibwagizo cha Peoples Power kinachotumiwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wakati wa mkutano wa Mweneykiti wa chama hicho, Freeman Mbowe
Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika (CHADEMA), akihutubia mkutano wa hadhara wachama hicho, wa Kampeni ya Vua Gamba Vaa Gwanda, uliofanyika mjini Tandahima mkoani Mtwar.
 Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe akihutubia mkutano wa hadhara wa Oparesheni Vua Gamba Vaa Gwanda, katika mji wa Chiungutwa jimbo la Lulindi mkoani Mtwara
 Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe akipandisha bendera ya chama hicho, wakati alipofungua Tawi jipya katika Mtaa wa Mkombozi mjini Newala. Kushoto kwake ni Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willibrod Slaa na kulia kwake ni Makamu Mwenyekiti, Zanzibar, Ali Issa Mohamed.
 
Picha zote na www.francisdande.blogspot.com

No comments:

Post a Comment