Hukumu ya kesi ya ubunge Ubungo kesho
Nimepokea
taarifa kwamba hukumu ya kesi ya uchaguzi dhidi ya ushindi wetu Jimbo
la Ubungo kesho tarehe 24 Mei 2012 itatolewa katika Jengo la MAHAKAMA
KUU (KIVUKONI-COURT No. 1) badala ya jengo ilipo mahakama ya kazi
(akiba) ambapo kesi iliendeshwa.
Kama tulivyotafuta kura pamoja,
tukapanga mstari kupiga kura pamoja na tukakesha kuzilinda pamoja
tujumuike pamoja kujua hatma ya kura zetu.
Hukumu ya kesi inatarajiwa
kuanza kusomwa SAA NNE ASUBUHI hata hivyo ni muhimu kuwahi mapema zaidi
asubuhi kwa ajili ya itifaki za kuingia mahakamani.
Chanzo: John Mnyika kwenye facebook
Nadhani kama bwana Mnyika au mashabiki wake wanataka kuingilia mahakama waseme tu wazi kwamba hawaheshimu utawala wa kisheria. Watambue kwamba Mahakama ni kama upanga wa kuwili na hivyo haishurutishwi kufanya maamuzi fulani kisa tu kuogopa makelele au vurugu za wahuni fulani. Nasema wahuni maana kuhamasisha wapiga kura waende mahakamanimkujua hatma ya kura zao ilihali kichwa cha ujumbe ni hakuna kesi kesho maana yake ni kutaka kufungulia kesi nyingine ya kusanyiko lisilo halali pia kama akishindwa kesi wafanye fujo au hata kumvamia hakimu. Jamani this is Tanzania fro Tanzanians siyo ya chama fulani au mtu fulani.
ReplyDelete