Gazeti
hili lilishuhudia msichana huyo mwenye umri wa miaka 17 (jina limehifadhiwa),
akikamatwa juzi saa 6 usiku Sinza nyumbani kwa Mama Angel.
Baada
ya kukamatwa, majirani wa Mama Angel ambao walishiriki msiba wa mtoto huyo,
walishirikiana kutaka kumuadhibu msichana huyo.
Inadaiwa
kuwa msichana huyo alisababisha kifo cha mtoto huyo wa miezi saba wakati Mama
Angel akiwa kazini Machi mwaka huu na kutoroka nyumbani hapo.
Kijana
wa mwenye nyumba hiyo, Ally Hasan alidai alikuwa wa kwanza kugundua kuwa mtoto
huyo amekufa baada ya Mama Angel kumpigia akimuomba kumuangalizia mtoto wake
huyo aliyekuwa amemuacha amelala.
Hasan
alidai alipoingia ndani ya chumba cha Mama Angel, alimkuta mtoto huyo akiwa
amelala na hakugundua kuwa alikuwa ameshakufa.
Kwa
mujibu wa madai ya Hasan, alitoa taarifa kwa Mama Angel kuwa mwanawe amelala na
mama huyo alimuomba amuamshe ndipo alipogundua kuwa amekufa baada ya kuona
haamki na kulazimika kutoa taarifa kwa mama mwenye mtoto alirudi nyumbani
haraka.
Alidai
kuwa mama wa mtoto huyo alipofika na kukuta mtoto ameshakufa kwa kushirikiana
na majirani walitoa taarifa Polisi na kumzika.
Hasan
alidai walianza harakati za kumtafuta msichana huyo wa kazi na kila
walipompigia simu yake, inadaiwa alikuwa akiwajibu kimkato huku akikiri kuwa
ameua mtoto huyo.
Naye
Mama Angel akizungumza na gazeti hili juzi usiku, alidai alifunga kula na
akaamua kufanya ibada kumuomba Mungu amuoneshe alipo msichana huyo, ndipo juzi
alipokuwa akipita eneo la Mwananyamala akiwa na mumewe, wakamuona akiwa mtaani.
Alidai
kuwa baada ya kumuona, walimkamata na wakampandisha katika teksi na kumpeleka
nyumbani kwao Sinza ili kumhoji zaidi.
Mwandishi
wa gazeti hili aliyekuwa eneo la tukio wakati dada huyo akishushwa,
alimshuhudia mfanyakazi huyo akilumbana na Mama Angel ambapo alimng’ata mama
huyo katika bega hali iliyozua tafrani baada ya majirani wa mama huyo
kujitokeza kwa wingi kumsaidia.
Baada
ya tafrani hiyo, msichana huyo wa kazi aliokolewa na wanaume waliokuwa eneo la
jirani ambao walimkamata na kumpeleka nyuma ya nyumba wakamzunguka na kumlinda
asidhurike na akinamama hao ambao wengi walikuwa wakidai kama msichana huyo
amesababisha kifo, iweje yeye asiuawe.
Mama
mzazi wa mtoto huyo akiwa mwenye uchungu, alisikika akieleza kuwa binti huyo
anapaswa kuchukuliwa hatua kwa mauaji ya mwanawe, huku akitaka kumuadhibu.
Hata
hivyo, wanaume waliokuwapo walizuia msichana huyo wa kazi asidhuriwe.
Baadhi
ya watu walipomhoji kuhusu kifo cha mtoto huyo, msichana huyo ambaye awali
alionesha ujeuri kwa kusema watamfanya nini, baadaye alikuwa mpole na kudai
mtoto huyo alimuacha ndani na hajui kilichomkuta.
Baada
ya saa moja, waliwasili askari Polisi wa Kituo cha Polisi Mabatini eneo la
Sinza waliomchukua na kuondoka naye huku wananchi waliokuwapo nje wakitaka
kumdhuru. Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela alipoulizwa,
alisema analifuatilia suala hilo na atatoa taarifa baadaye.
Chanzo: HABARILEO
No comments:
Post a Comment