Thursday, May 24, 2012

Hatimaye Nchunga aachia ngazi Yanga

Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Lloyd Nchunga amejiuzulu.

Klabu hiyo sasa inaongozwa na Bodi ya Wadhamini iliyomjumuisha Francis Kifukwe, Yusuf Manji na Mama Shadya Karume.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, wanachama wapatao 600 wakiongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Ibrahim Akilimali pamoja na Mwenyekiti wa Vijana Bakili Makele walitangaza kumng’oa madarakani Mwenyekiti wao Nchunga.

Shirikisho la Soka nchini (TFF) lilikataa mapinduzi hayo kwa vile yako kinyume na Katiba. 

Tayari wajumbe saba wa Kamati ya Utendaji ya Klabu hiyo wametangaza kujiuzulu



No comments:

Post a Comment