Thursday, April 5, 2012

Godbless Lema avuliwa ubunge

Mahakama Kuu Kanda ya Arusha leo imemvua ubunge aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema.

Muda mfupi baada ya uamuzi huo, Lema amedai kuwa, uamuzi huo ulipangwa.

Kwa mujibu wa Lema, Jaji ametoa uamuzi huo kwa amri ya Serikali.

Lema amesema, atazungumza na viongozi wa Chadema ili wajue nini cha kufanya na kuwaeleza wananchi wafanye nini.

Amedai kuwa, kwa kuwa Mahakama imekandamiza haki, wananchi wataipata haki hiyo porini.

Habari zaidi baadaye.

1 comment:

  1. Pole sana Mheshimiwa Lema, nafikiri pamoja na kuwa ni kweli matusi ulitukana, kauli chafu ukatoa, ukadhalilisha kama wanavyofanya CCM (Lusindes) na hawavuliwi ubunge, hupaswi kupata adhabu hiyo. Ubunge ni wako kijana unakubalika ila ninachokushauri, kauli za kutishia "kuingia porini" "kuingia msituni" achana nazo bwana maana zinakupotezea uaminifu ambao wananchi wanao juu yako, wanataka uwatetee lakini kwa njia za hoja, na kufuata misingi ya sheria ya nchi ambayo matokeo yake ndio amani wananchi wanayoburudika nayo. Usijali waache warudishe mprira kati, mpira utaelekea goli lao to very soon.

    ReplyDelete