Lulu
Inadaiwa kwamba, Lulu aligombana na Kanumba ambaye inasemekana alikuwa mpenzi wake baada ya kukutwa akiongea na mwanaume mwingine, kwenye simu.
Karibu kila kona ya Jiji la Dar es Salaam, mazungumzo yalikuwa juu ya msiba huo, huku wengine wakionekana kuguswa kutokana na ukweli kwamba, Kanumba alikuwa kipenzi cha wengi kutokana na umahiri wake katika uigizaji.
NYOTA ya msanii maatufu wa filamu ndani na nje ya Tanzania, Steven Charles Kanumba imezimika ghafla.
Hakuna aliyetarajia kusikia taarifa mbaya kuhusu kifo cha kijana huyo aliyeaga dunia akiwa na umri wa miaka 27!
KWA MUJIBU WA MSAIDIZI WA MAREHEMU STEVE KANUMBA, (BWANA SETI) , ELIZABETH MICHAEL MAARUFU KAMA LULU ALIKUJA NYUMBANI KWA KANUMBA KUKAWA NA KAUGOMVI, WAKAINGIA CHUMBANI.
WAKATI WAKIWA HUKO, BAADA YA MUDA, LULU ALITOKA NA KUMUITA YEYE KUMUAMBIA KANUMBA KAANGUKA.
ALIPOENDA AKAMKUTA KAANGUKA, AKAENDA MUITA DAKTARI WA KANUMBA ALIPORUDI HAKUMKUTA LULU.
BINTI HUYO MWENYE UMRI WA MIAKA 18 AMEKAMATWA, YUKO POLISI OSTERBAY, DAR ES SALAAM.
Inadaiwa kwamba, Lulu aligombana na Kanumba ambaye inasemekana alikuwa mpenzi wake baada ya kukutwa akiongea na mwanaume mwingine, kwenye simu.
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Charles Kenyella alinukuliwa akisema Kanumba alikuwa katika `ugomvi’ na msanii wa kike anayekuja juu katika filamu, Elizabeth Michael `Lulu’ anayedaiwa alikuwa mpenzi wake.
Karibu kila kona ya Jiji la Dar es Salaam, mazungumzo yalikuwa juu ya msiba huo, huku wengine wakionekana kuguswa kutokana na ukweli kwamba, Kanumba alikuwa kipenzi cha wengi kutokana na umahiri wake katika uigizaji.
Kanumba, alisoma katika Shule ya Msingi Bugoyi kisha akaingia Mwadui Seminari iliyopo Shinyanga na kukamilisha masomo yake ya O-Level Shule ya Dar es Salaam Christian Seminary.
Masomo ya kidato cha tano na sita alichukulia Jitegemee .
Alijiunga na Kaole Sanaa Group ya Dar es Salaam kama muigizaji na kuanza kutokea katika vipindi vya kuigiza vya televisheni za TBC na ITV ikiwemo ‘Jahazi’, ‘Dira’, ‘Zizimo’, ‘Tufani’, ‘Sayari’, ‘Taswira’, ‘Gharika’ na ‘Baragumu’.
Nenda Kanumba, wengi wanakulilia.
No comments:
Post a Comment