Tuesday, January 17, 2012

Mamia wamuaga Regia Mtema viwanja vya Karimjee

Askari wa Bunge la Tanzania wakiwa wameubeba mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum , Regia Mtema (Chadema), kuupeleka sehemu iliyokuwa imendaliwa kwa ajili ya waombolezaji kutoa heshima za mwisho katika Viwanja vya karimjee jijini Dar es Salaam.


Marehemu Regia (32) anasafirishwa leo hadi Morogoro kwa ajili ya maziko.

Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal akitoa heshima za mwisho kwa marehemu Regia Mtema, leo katika viwanja vya Karimjee.
Spika wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya Bunge
Makamu wa Rais, Dk Bilal akisalimiana na Andrew Chenge katika viwanja vya Karimjee leo.




Gari alilokuwa akiendesha Regia Mtema aina ya Toyota Land Cruiser.


Inadaiwa kuwa gari hilo lilipinduka mara 7 Jumamosi saa 5 asubuhi eneo la Ruvu mkoani Pwani baada ya Regia kuamua kulipeleka nje ya barabara kuepuka kugongana uso kwa uso la lori aliloliona ghafla wakati anataka kulipita gari lingine.

No comments:

Post a Comment