Saturday, December 3, 2011

Buriani 'Mr Ebbo'

MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Abell Motika ‘Mr. Ebbo’ amefariki dunia.

Msanii huyo aliaga dunia usiku wa kuamkia jana kwenye Hospitali ya Misheni iliyopo Usa River, wilayani Arumeru nje kidogo ya Jiji la Arusha.

Mr. Ebbo ambaye alikuwa maarufu kwa nyimbo za Kimasai alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya mapafu kwa muda mrefu.

Imeelezwa kuwa ndugu na jamaa walihangaika na matibabu kwenye hospitali mbalimbali za ndani na nje ya nchi, lakini hakukuwa na mafanikio ya kuridhisha.


Akizungumza na gazeti hili, kaka wa marehemu, Julius Motika alisema alikuwa akipata nafuu kwa muda fulani na baadaye hali yake alibadilika.


Motika alisema kwa sasa mwili wa marehemu uko katika Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru mjini Arusha na mipango ya mazishi inaendelea ikiwa ni pamoja na kuwasubiri baadhi ya ndugu ambao wapo nje ya nchi.


Alisema marehemu ameacha mjane na watoto watatu.

Mara nyingi 'Mr Ebbo' alifanyia shughuli zake mkoani Tanga, lakini atazikwa Arusha.


Baadhi ya nyimbo zilizompa umaarufu Mr. Ebbo aliyeanza kusikika mwanzoni mwa miaka ya 2000 ni ule wa Mi Mmasai, Kamongo na Bodaboda, vibao ambavyo vyote vilikuwa kivutio kikubwa kwa mashabiki.


Chanzo:Gazeti la HABARILEO

No comments:

Post a Comment