Friday, December 2, 2011

Buriani David Wakati

David Wakati enzi hizo


MKURUGENZI mstaafu wa iliyokuwa Redio Tanzania ambayo sasa ni sehemu ya Shirika la Utangazaji (TBC), David Wakati (pichani) amefariki dunia jijini Dar es Salaam jana baada ya kuugua muda mrefu maradhi ya kisukari.


Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Clemence Mshana alithibitisha kifo hicho jana na kusema kuwa alifariki jana asubuhi wakati akitibiwa katika Hospitali ya Regency.


Alisema Wakati alilazwa katika hospitali hiyo tangu Ijumaa baada ya kuugua kwa muda mrefu maradhi hayo pamoja na kiharusi.


Kwa mujibu wa Mshana, utaratibu wa mazishi unafanyika nyumbani kwake Masaki.


Wakati alikuwa mtangazaji mahiri wa redio na Mkurugenzi mwanzilishi wa TBC na iliyokuwa Redio Tanzania, sasa TBC Taifa.

Chanzo: Gazeti la HABARILEO

1 comment:

  1. This blog very interesting but you can also try these ..www.jigambeads.com and ..www.tanzaniakwetu.com for popularity and more advert to advertise. Thanks

    ReplyDelete