Thursday, November 10, 2011

Mbowe- Nijisalimishe naogopa nini, Mbowe wanamjua wanamsikia?

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, akiwasiil katika Ofisi za Polisi Mkoa wa Arusha kwenda kujisalimisha.
Mbowe akienda ofisini kwa RPC jana Jumatano.

Mbowe akizungumza na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Simon Sirro ofisini kwa kamanda huyo.

"Sasa mimi nawaambia nakwenda polisi mwenyewe, si kwa sababu ya eti naogopa, eti nakwenda kujisalimisha, nijisalimishe kwani naogopa nini.


Nimetoroka wapi, kwa sababu hata tukio lenyewe walipokuwa wanakamata watu sikuwepo mimi uwanjani.


Lakini wengine wanasema Mbowe alikuwepo, ametoroka na gari lake, akakimbia. Mimi Mbowe nikimbie! Hivi wanamjua Mbowe, wanamsikia Mbowe?" Nukuu ya kauli ya Freeman Mbowe jana kwa waandishi wa habari mjini Arusha.

No comments:

Post a Comment