Thursday, November 17, 2011

Maisha yanaendelea

MKUU wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro alikuwa ndani ya gari hili akivuka kutoka katika mradi mkubwa wa kilimo cha umwagiliaji uliopo Naming'ong'o katika kijiji cha Nkala kata ya Chitete wilayani Mbozi.


Bw.Kandoro akipita katika maji wamachinga jijini Mbeya walikuwa wakipambana na Polisi na kusababisha vurugu kubwa.


Kandoro alilazimika kukatisha ziara Mbozi na kurudi jijini Mbeya mjini. Mkuu wa Mkoa wa Mbeya akizungumza na waandishi wa habari kuhusu miradi ya kijamii alipotembelea vijijini wakati huo huo jijini Mbeya vurugu ikiibuka kati ya Machinga na Polisi.


Hawa ni baadhi ya wananchi ambao Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Bw. Kandoro alikutana nao alipokuwa katika ziara yake Mbeya vijijini.


Mwananchi akichota maji yanayopita katika mto.


Picha, Habari kwa hisani ya blog ya Mbeya yetu

No comments:

Post a Comment