Tuesday, November 15, 2011

Diamond ana chale 21

CHALE 21 alizochanjwa mwanamuziki wa kizazi kipya Bongo, Naseeb Abdul ‘Diamond’ zinadaiwa kuwapa mshtuko watu wake wa karibu na kuanza kuzitafsiri kwa namna tofauti huku wengine wakizihusisha na ushirikina.


Inadaiwa kuwa, chale zimemsaidia mume mtarajiwa wa Wema Sepetu kung’ara katika anga ya bongo flava nchini na kwingineko sanjari na kuwapeleka mbio wasichana a.k.a mademu.


“Unajua wenzake wanasema zile chale zinamsadia jamaa kwenye nyimbo zake kuwa bora, lakini pia zinamfanya apendwe na mademu, we si unaona mwenyewe?”

Diamond ameshadaiwa kuwa na uhuasiano wa kimapenzi na mastaa na wasio mastaa takribani watano bongo, amewahi kukiri sanjari na kukanusha tuhuma hizo.


Mastaa wanaodaiwa kuvunja amri ya sita na Diamond ni Rehema Fabian (Miss Kiswahili 2008), Jacqueline Wolper (msanii wa filamu), Upendo Moshi ‘Pendo’ (Mshiriki wa Maisha Plus), Natasha (msanii wa nyimbo za bongo flava) na sasa Wema Sepetu (Miss Tanzania 2006) na sasa wanatajwa kuwa ni wachumba.


Diamond anasema nini kuhusu chale zake 21?


"Si kweli bwana, chale kweli ninazo ila sababu siyo eti nyimbo zangu zing’are au mademu wanishobokee"


"Nilipokuwa mtoto niliwahi kusumbuliwa sana na ugonjwa wa kichomi cha mara kwa mara, ikafika wakati nikapelekwa kwa tabibu wa tiba asilia ndiyo nikachanjwa chale, kwa hiyo nimekua nazo"


Picha kwa hisani ya blog ya bongoflavalink

1 comment:

  1. DUH KAMA VP WANGU TUPIA HATA TATOO JUU YA HIZO CHALE MAANA ZINAKUSHUSHIA HADHI YAKO

    ReplyDelete