KUNA taarifa kwamba Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Kabwe Zitto hivi sasa anatolewa Hospitali ya Taifa Muhimbili,jijini Dar es Salaam anapelekwa India kutibiwa.
Kwa siku kadhaa sasa, hali ya Mbunge huyo machachari si nzuri,kwanza alilazwa hospitali ya Agha Khan, Dar es Salaam, na baadaye akahamishiwa Muhimbili.
Jana, kulikuwa na uvumi kupitia ujumbe mfupi wa simu za mkononi(sms) kwamba, Zitto, amefariki dunia lakini ukweli ni kwamba, yupo hai na alikuwa amelazwa katika wodi ya wagonjwa wanaohitaji uangalizi zaidi(ICU).
Taarifa kutoka Muhimbili, zimeeleza kuwa,Zitto,amekutwa na vijidudu 150 vya malaria na anaendelea vizuri chini ya uangalizi maalumu wa madaktari.
Gazeti la Serikali la HABARILEO la leo limemnukuu Msemaji wa hospitali hiyo, Jezza Waziri, akisema, wataalamu wanaomtibu Zitto walibaini kwamba anasumbuliwa na malaria na kukutwa na vijidudu hivyo mwilini.
“Tofauti na jana (juzi) alipofikishwa hapa, leo (jana) hali yake inaendelea vizuri na yuko chini ya uangalizi maalumu akiendelea na matibabu,” alisema Waziri.

No comments:
Post a Comment