Friday, July 22, 2011

Yanga shangwe bungeni Dodoma

DAKIKA chache zilizopita, kulikuwa na 'kituko' cha aina yake bungeni mjini Dodoma baada ya mmoja wa wabunge kuomba mwongozo wa Mwenyekiti wa Bunge, George Simbachawene, na kuhoji kwamba, timu ya Simba ya Dar es Salaam imechukua kombe la Kagame mara 6, Yanga imetwaa kombe hilo mara 4 tu, kwa nini wenzao (Yanga) waitwe bungeni wakati Simba haijawahi kuitwa hata mara moja?


Simbachawene kamjibu kwamba, mwongozo wake ni kuwa, Yanga ndiyo mabingwa wa ligi Kuu Tanzania bara, na ni mabingwa wa kombe la Kagame, na siku ya fainali, yanga iliifunga Simba bao moja.


Mbunge huyo wa Kibakwe mkoani Dodoma aliuliza kama aliyepiga krosi iliyozaa bao alikuwa hapo bungeni mjini Dodoma pamoja na wachezaji wengine wa Yanga, akasema safi sana, kauliza pia kama mfungaji wa bao hilo, Keneth Asamoah alikuwepo, akasema safi sana.


Baada ya kusema hayo, Mwenyekiti huyo wa Bunge aliagiza shughuli za Bunge ziendelee, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe akasimama kusoma bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2011/2012.


Wakati anaanza kusoma bajeti hiyo, Membe, alisema, anafichua siri leo kuwa na yeye ni mpenzi mkubwa wa Yanga, kawapongeza kwa kutwaa kombe la Kagame.

No comments:

Post a Comment