Thursday, October 7, 2010

Umekanyaga mpira wa Oxygen

Mgonjwa mahututi alikuwa hawezi kuongea, alipofikishwa hospitalini akawekewa oxygen.
Basi mchungaji akaja kumuombea. Wakati akiombewa, yule mgonjwa akachukua kalamu na karatasi, Akaandika haraka haraka na akampa yule Mchungaji.
Ambaye badala ya kuisoma ile karatasi, akaitia kwenye mfuko wa joho na kuendelea na maombi hadi yule mgonjwa, akakata roho.
Mchungaji hakuisoma ile karatasi alidhani ni wosia wa marehemu.
Alisubiri baada ya mazishi kwenye kikao cha ndugu akasema;
"KUNA KITU NILIPEWA NA MAREHEMU SIKU NILIYOKUA NAMUOMBEA"
Akampa mmoja wa wanandugu aisome. Haya ndiyo yaliyokuwa yameandikwa na yule mgonjwa:
"UMEKANYAGA MPIRA WA OXYGEN, NAKOSA HEWA"

No comments:

Post a Comment