Wednesday, June 16, 2010

Nguvu za kiume (2)

Tunatakiwa kuajitambua sisi wenyewe kwanza, tukijua historia na mazingira yetu ya kimapenzi.
Kwa wanaume ambao wamebanwa sana kikazi na hufanya mapenzi mara moja moja, hukabiliwa na tatizo la kukosa msisimko kwa sababu miili yao imezoea.

Sasa ili kuifanya ichangamke lazima waanze kuirejesha kwa kufanya mapenzi mara kwa mara na kwa raundi chache. Kisha wanatakiwa kufanya mazoezi na kula vyakula, vinywaji vyenye nguvu ili kujipa nguvu.

Pia kama mwanaume ameishi na mwanawake kwa muda mrefu na amekuwa na desturi ya kufanya mapenzi mara kwa mara katika mazingira yale yale anaweza kukumbwa na kasoro hiyo.

Hivyo anashauriwa kubadili mazingira ya kufanyia mapenzi, kupeana mahaba mapya, kuamsha mapenzi kwa kujaliana, pia kuondoa fikra zote zenye kukinaisha ikiwa sambamba na kuzingatia usafi wa mwili.

Yakifanyika hayo mwili utaitikia taarifa ya akili na nguvu zitapatikana. Kwa wanaoshindwa kurudia tendo wanatakiwa kufuata kanuni hizo hapo juu. Jambo kubwa ni suala la kuuzoeza
mwili.

Usiulazimishe kuanza mara moja kwenda mara nyingi wakati mapenzi yako yamekuwa ya kuiba mpaka baba alale na wakati mwingine muda wako wa kutoka kazini umebana na hivyo kukufanya ufanye mapenzi ya chap chap kila siku.

Ukiwa mtu wa namna hii haiwezi ikatokea siku moja ghafla tu ukafanya mpenzi mara tatu bila kuchoka.
Pia inawezekana mwanaume akashindwa kurudia tendo si kwa sababu hana nguvu bali hapewi ushirikiano wa kutosha toka kwa mpenzi wake.

Hivyo wakati wa kutafuta uwezo wa kwenda raundi nyingi ni vema usaidizi wa mwanamke ukatolewa, isitokee kupokea lawama tu za “huwezi, sijatosheka” kwa sababu hizo ndizo zinazowafanya wanaume washindwe kabisa kwa hofu kuwa wanaaibika.

Mawazo ya kuaibika yanapopewa kipaumbele huufanya uume kuzidi kusinyaa, kwa maana hiyo ni vema kuyatupilia mbali na kuacha kujihukumu.

Pia kuna hitilafu ya wakati wa kuridhishana, inaweza kutokea mwanamke akawa kamaliza raundi yake ya kwanza, wakati anaingia msisimko wa pili mwanaume anafika kileleni, kinachotokea ni mwanamke kumlazimisha mwanaume arudie tendo kwa muda mfupi tangu amalize, jambo ambalo ni vigumu.

Sasa ikitokea mwanaume kachezewa na hana msisimko anapata hofu kuwa hawezi, ikijengeka hivyo hata iweje jambo halitawezekana tena. Hivyo ni bora kupeana muda wa kupumzika kabla ya hatua ya pili ya mchezo.

Pale inapotokea hamasa ya kurudia haipo fikra za mwanaume zisipewe nafasi ya kushindwa kwa kuwa nyakati, mchoko, makujukumu, hofu za maisha na mambo kama hayo yanapokuja katika siku ya kustarehe ni wazi kuwa kiwango cha ufanyaji mapenzi kitakuwa chini na hali hii huwatokea wanaume wote, hata walio hodari wa kwenda raundi 10 kwa siku.

Sambamba na hilo wanawake wanashauriwa kutoonesha kujali pindi inapotokea hali hiyo, badala yake wawaambie wenzao kuwa siku hiyo inatosha hata kama hawajatosheka, lengo ni kuondoa hofu ambayo ndiyo msingi wa wanaume kuishiwa uwezo wa kufanya mapenzi.

Hata hivyo maudhi, kufanya mapenzi na usiyempenda, msongo wa mawazo na kutokuaminiana huchangia kupoteza msisimko wa kuwa ‘kidume’.

Chochote ambacho unataka mwili wako ukifanye lazima uuzoeze. Ukizoea kuamka saa 12 asubuhi mwili utatii kanuni hiyo.Na ukizoea kufanya mapenzi kila siku mara mbili au tatu hali itakuwa hivyo.

No comments:

Post a Comment