Tuesday, June 15, 2010

Ng'ombe chupuchupu bwawani


NG’OMBE aliyepotea amejikuta akiogelea bwawani Dorset, Uingereza.
Ng'ombe huyo alikimbia kutoka katika shamba lakini haijafahamika kwa nini alifanya hivyo.

Wafanyakazi katika bwawa hilo ilibidi wafanye kazi ya ziada kuokoa maisha ya mnyama huyo.

Ng'ombe huyo anaitwa Daisy,alitoroka shambani Motcombe, akaanza kuzurura katika eneo la nyumba ya jirani.

Kikosi cha zimamoto kutoka Shaftesbury, kundi la kuokoa wanyama kutoka Poole, daktari wa wanyama na gari maalum la kufanyia kazi hiyo, vilitumika katika operesheni ya kumuokoa.

Ofisa wa zimamoto Michael Stead, amesema, ng’ombe huyo aliyekuwa hajafikisha hata umri wa mwaka mmoja angeweza kukaa majini humo kwa saa kadhaa bila kudhurika.
“Kitu cha ajabu, alionekana kuwa mtulivu,” alisema Stead, “lakini alifanya matata kidogo tulipotaka kumfunga kamba ili kumtoa.”
Waokoaji ilibidi wamchome dawa ya usingizi ili wamuondoe kuondolewa majini na kurudishwa shambani.

“Alionekana mchovu kama vile amelewa, bila shaka kwa kushangaa na kile kilichokuwa kimemtokea,” alisema ofisa mmoja wa zimamoto.
“Nimeshiriki katika matukio kadhaa yanayohusu ng’ombe lakini hili limenishangaza. Hata hivyo, tunafurahi hakupata madhara yoyote.” alisema.

No comments:

Post a Comment