Mke na mume waliobarikiwa kuwa na mtoto mmoja mdogo walipendana sana na daima walitaka kudhihirisha upendo wao kwa watu ikiwa ni pamoja na kushikana mikono, kuitana majina matamu kama "honey, Darl, Dear, Switiiii" nk nk.
Siku zote mmoja wao akiwa anatoka huwa ana muaga mwenzake na mtoto kwa staili ya busu na kukumbatiana. Mtoto alizoea hali ya mapenzi ya wazazi.
Siku moja wapendanao hao waligombana usiku na kurushiana kauli zisizofaa kuhusu mapenzi yao.
Mke akakasirika sana, wakati anakwenda kazini asubuhi, hakutaka hata kumuaga mumewe, wakati huo 'hazbendi' wake alikuwa sebuleni na mtoto wao.
Mama akambusu mtoto tu, akafungua mlango na kuanza kuondoka ....
Lakini ghafla mtoto akamuuliza: "mamiii...." mama alipogeuka na kuitika, "yes mai dia": mtoto akauliza: ...."Mamiii why today you don't want to kiss mai Dadiii...., are u okei??"
Mtoto akamkimbilia mama na kushika mkono kumrudisha ndani ili ambusu japo kidogo tu "dadiii wake".
Mama akajisikia aibu sana nafsini mwake, akarejea na kumbusu "Dadiii"!japo kwa shingo upande...Dadiii nae pia ikamwingia hiyo!.
No comments:
Post a Comment