Tuesday, June 29, 2010

Kwa ni PCM wengi wanaenda Commerce?

KUNA mdau kanitumia hii
Katika miaka ya karibuni, imekuwa "fashion" kwa wanafunzi waliosoma PCM form 6 kujiunga na vyuo vya biashara, yaani, kusoma B.Comm na BAF (Bachelor of Accounting and Finance).
Utakuta hata wale waliopasua form 6 kwa kupata Div I kali (chini ya 6 pts) wanaenda kusoma hayo masomo.
Hoja hapa si kuwa masomo haya ni mabaya ila ni kuuliza tu, nini chanzo kunichowafanya wachague field hii?

Ni wanafunzi hawa hawa ambao tulitarajia wawe wahandisi na wavumbuzi mahiri ambao wangeweza "kusaidia" taifa katika karne hii ya uvumbuzi (invention and innovation era).
Kwa nini wasisome Electrical Engineering, Telecomm, Computer Science, Civil Engineering?

No comments:

Post a Comment