Wednesday, November 25, 2009

Amnyonga mkewe usingizini

MWANAUME nchini Uingereza, Brian Thomas (59) anadaiwa kumnyonga mkewe, Christine (57) wakati wakiwa wamelala.
Brian anadaiwa kumyonga mkewe wakati anaota akidhani alikuwa anapambana na mwizi aliyewavamia kwenye gari lao.
Mahakama nchini humo imeelezwa kwamba, Brian na Christine wameishi kwenye ndoa kwa miaka 40.
Brian alimuua mkewe usiku wa manane kwenye gari lao wakati wakiwa katika safari ya mapumziko.

Mahakama iliambiwa kuwa Brian aliota ndoto kuwa mwizi amevunja na kuingia ndani ya gari lao, akaota
anapambana na mwizi huyo na matokeo yake kumbe alikuwa akimkaba kipenzi chake cha tangu utotoni.
Mahakama ya mji wa Swansea iliambiwa kuwa Brian alikuwa akisumbuliwa na matatizo sugu ya usingizi na alikuwa hajitambui anamkaba mkewe.

"Hii ni kesi ya aina yake, sio ya kawaida", alisema mwendesha mashtaka Paul Thomas.

"Wataalamu wa usingizi wamemfanyia uchunguzi Brian na wametoa ripoti kuwa hakufanya kitendo hicho kwa kukusudia".

"Hawezi kutiwa hatiani kwa kitendo chake", alisema mwendesha mashitaka huyo.

Mahakama iliambiwa kuwa Brian na mkewe walionekana siku ya tukio hilo wakila nyama na chipsi pamoja mbele ya gari lao.

Siku hiyo walienda kulala mapema lakini usiku wa manane, Brian alianza kuota ndoto amevamiwa na mwizi.
Polisi walimkuta Christine akiwa amekufa baada ya kukabwa sana koo.
Wanandoa hao ambao wana watoto wawili wa kike na walikuwa wapo kwenye hatua za mwisho za kuanza likizo kwenye meli kubwa ya kifahari kuzunguka bahari ya Mediterranean kusherehekea miaka 40 ndoa yao.

No comments:

Post a Comment