Thursday, September 17, 2009

Ni hatari kulala na mpenzi wako

WANASAYANSI nchini Uingereza wameonya kwamba kitendo cha wapenzi kulala kitanda kimoja ni cha hatari kwa afya zao na pia huweza kuhatarisha uhusiano wao.

Wanasayansi hao wamesema kuwa kitendo cha kulala kitanda kimoja humsababishia mtu kupata usingizi duni.
Kwa mujibu wa wanasayansi hao hali hiyo inaweza kusababisha magonjwa mbali mbali yanayotokana na ukosefu wa usingizi kama vile magonjwa ya moyo na msongo wa mawazo.

Wanasayansi hao wanasema, kwa wastani wapenzi wanapolala pamoja huwa na usingizi duni kwa asilimia 50 kwa sababu ya kuamshana amshana na hali hiyo huwa tofauti wakati wanapolala peke yao.

Watu kukoroma, kugonga gonga meno na kujigeuza geuza kitandani, kuamka usiku kwenda chooni ni miongoni mwa sababu zinazowanyima wapenzi usingizi bora.

Wanasayansi hao walisema kuwa wapenzi kulala kitanda kimoja huchukuliwa kitamaduni kuwa ni kuonyesha mapenzi na upendo wakati kitendo cha wapenzi kulala vitanda tofauti huonekana si jambo sahihi katika tamaduni.

Wakiongea katika tamasha la sayansi la Uingereza, wanasayansi hao waliwashauri watu wachukue hatua mapema kabla ya afya zao kutetereka au uhusiano kuvunjika.

Dr Neil Stanley, mtaalamu wa mambo ya usingizi toka hospitali ya chuo kikuu cha Norfolk and Norwich University ambaye hulala kitanda tofauti na mkewe alisema
" Usingizi ni kitu chenye uchoyo, hakuna mtu anayeweza kushea usingizi".

Akiongelea majaribio ya kisayansi waliyoyafanya kwa pea 40 za wapenzi Dr Stanley alisema
"Watu hujihisi wanapata usingizi bora wakilala pamoja lakini ushahidi wa kisayansi unaonyesha tofauti".

Kama haiwezekani kulala vitanda tofauti, Dr Stanley alitoa ushauri wa kununua kitanda kikubwa zaidi na kila mtu atumie shuka lake.

3 comments:

  1. Unajua utafiti huu umeangalia `kukosa usingizi' ukaacha `kudumisha upendo'
    Wanandoa mnapolala pamoja mnadumisha upendo,mnajenga ile falsafa ya mwili mmoja, kiasi kwamba mmoja akiondoka unajihisi umekosa sehemu ya mwili.
    Unajua tafiti nyingine ni za kibinafsi, yaani upate, ufaidi wewe tu, inabidi wakati mwingine ujitolee ili mwishowe mpate wote.

    ReplyDelete
  2. Hamna kitu nnachopenda kama kulala na mume wangu...raha kupitilizaaaa!
    hao wanasayansi wamekosa mtu wa kulala nae!

    ReplyDelete
  3. kaka kumbe na wewe unablogisha siku hizi? safi sana, kazi nzuri, na tupo pamoja! issa moscow

    ReplyDelete