Friday, September 4, 2009

Mbowe awapasha wapinzani wa Chadema

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe, amewataka watu na vyama vya siasa vinavyolaani mchakato wa kuwapata viongozi wa kitaifa wa chama hicho wasikifundishe demokrasia chama hicho.

Mbowe amewataka watu hao watumie muda wao kutibu kansa inayotafuna vyama vyao.

Mbowe ametoa msimano huo jana Dar es Salaam wakati anafungua mkutano mkuu wa chama hicho.

Amesema,Chadema ni wamoja na wataendelea kuwa wamoja, wanaheshimiana ila watatofautiana katika baadhi ya hoja za msingi huku wakiamini kuwa Chadema ni muhimu kuliko kiongozi yeyote.

“Wengine eti wanatushauri namna ya kujenga demokrasia ndani ya chama chetu kwa kisingizio kuwa kuna mpasuko, sasa nawaambia muda wanaotumia kutushauri sisi wautumie kutibu kansa ndani ya vyama vyao kwani sisi Chadema ni wamoja,” alisema Mbowe.

Mwanasiasa huyo amesema Chadema ya sasa si ya viongozi wa meza kuu,ni ya Watanzania wote, na kamwe viongozi waliopo madarakani kwa sasa hawatasaliti imani waliyonayo Watanzania kwa chama hicho.

“Ni juu yetu sisi viongozi mimi Mbowe, Zitto (Kabwe) na wengine kuhakikisha hawawasaliti Watanzania,” amesema Mbowe.

“Unapoona Chama cha Mapinduzi na vyombo vyake vya habari vimeshahabikia na kutushauri namna ya kuendesha demokrasia ujue lengo lao ni kutaka kukivuruga chama chetu.”amesema.

No comments:

Post a Comment