ALIYEKUWA Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala Benki Kuu Tanzania,Amatus Liyumba, jana alidai mahakamani kuwa,Bodi ya benki hiyo iliridhia malipo kwa ajili ya mabadiliko ya ujenzi wa majengo pacha ya taasisi hiyo
ya Serikali.
Liyumba ameshitakiwa akidaiwa kutumia vibaya madaraka na kuisabababishia Serikali hasara ya zaidi ya bilioni 200 kupitia ujenzi wa majengo hayo jijini Dar es Salaam.
Liyumba leo ameonyesha kushangaa kuelezwa kuwa alifanya mabadiliko ya ujenzi wa majengo hayo bila kupata ruhusa ya bodi ya BoT.
Mshitakuwa huyo amehoji,kama Bodi ya BOT haikutoa ruhusa hiyo fedha zote hizo zilitoka wapi.
“It’s a useless board basi!” amesema Liyumba kwa mshangao katika Mahakama ya Hakimu Mkazi,Kisutu, Dar es Salaam.
Mwendesha mashitaka,Justus mlokozi jana alisoma maelezo ya awali ya kesi hiyo sanjari na kusoma mashitaka mapya yanayomkabili Liyumba.
Baada ya Mlokozi kusoma mashitaka,Liyumba alitakiwa aieleze mahakama anayakubali au anayakataa mashitaka hayo.
Alikiri kuwa alikuwa na wadhifa huo, na aliyakubali majina majina yake.
Mwendesha mashitaka aliieleza mahakama kuwa,Liyumba alidaiwa kuwa aliajiriwa na Benki Kuu ya Tanzania mwaka 1973 na alikuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa benki hiyo tangu mwaka 1979 hadi mwaka 2008
alipostaafu.
No comments:
Post a Comment