Thursday, September 3, 2009

Bilionea wa Chelsea yupo Arusha

Abramovich akiwa na mpenzi wake, Dasha.
Boti ya kifahari ya bilionea Abramovich
MMILIKI wa klabu ya Chelsea ya Uingereza, Roman Abramovich(42) yupo Arusha nchini Tanzania kutalii na kupanda Mlima Mrefu kuliko yote Afrika, Kilimanjaro.
Mrusi huyo anayeshika nafasi ya 11 kwa utajiri duniani aliwasili jana usiku katika uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro (KIA).

Hivi karibuni bilioni huyo alinunua boti mpya kubwa kuliko zote duniani yenye viwanja viwili vya helikopta na mfumo wa ulinzi kama wa
kijeshi.

Boti hiyo iliyotengenezwa kwa siri mjini Hamburg, Ujerumani iliwafanya watu wengi wabaki wakiikodolea macho kwa mshangao wakati ilipokuwa ikiingia baharini kwa mara ya kwanza.

Boti hiyo mpya yenye urefu wa mita 211 ilimgharimu Abramovich kiasi cha dola milioni 495. Inadaiwa kwamba utajiri wake unatokana na biashara ya mafuta.

Inadaiwa kwamba boti hiyo ya Abramovich imekuwa ni boti ndefu kuliko zote duniani, imeizidi boti ya tajiri wa dubai Sheikh Mohammed bin Rashid Al Maktoum ambayo ilikuwa ikiongoza kwa urefu duniani ikiwa na urefu wa mita 198.

Boti mpya Abramovich ina kila kitu cha starehe kuanzia mabwawa ya kuogelea, spa ya kifahari na hata ina submarine yake ndogo.

Kwa mujibu wa tovuti ya nifahamishe.com, ili kuhakikisha ulinzi wa Abramovich boti hiyo ina mfumo wa ulinzi sawa na wa kijeshi wa kuzuia makombora na
pia ina madirisha yenye vioo visivyopitisha risasi.

Boti hiyo mpya iimepewa jina la Eclipse, itaungana na boti zingine tatu kubwa za bilionea huyo katika shoo yake ya utajiri.

Kila boti ya Abramovich ina kazi yake maalumu, wakati boti yake ya Pelorus yenye urefu wa futi 377 huitumia kwa sherehe zake na marafiki zake, boti yake inayoitwa Ecstasea yenye urefu wa futi 228 huitumia kwenye safari zake za kitalii.
Boti nyingine iitwayo Sussurro yenye urefu wa futi 161 huitumia kwa safari fupi fupi na kuwaazima marafiki zake wajidai nayo kwa muda.

No comments:

Post a Comment