Thursday, August 20, 2009

Wanafunzi ruksa kutumia past papers

BARAZA la Mitihani la Tanzania(NECTA) limewaruhusu walimu na wanafunzi watumie karatasi za mitihani iliyopita kwa matumizi ya kielimu na si biashara.

Hivi karibuni, baraza hilo lilisema litamchukulia hatua kali za kisheria mtu yeyote atakayebainika kuchapisha au kuuza karatasi hizo bila idhini yake.

“Baraza linapenda kuufahamisha umma kwamba karatasi hizo zinaweza kutumiwa na walimu au wanafunzi kwa matumizi ya ki-elimu na si biashara,” Necta imesema katika tangazo alilotoa Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Dk Joyce Ndalichako.

No comments:

Post a Comment