Friday, August 21, 2009

Uroda juu ya meza ya bwana

WANAIJERIA wawili, mtu na mkewe, ambao walikuwa na nia ya kuyaamsha mapenzi yaliyopooza katika ndoa yao na kuamua kufanya mapenzi ndani ya kanisa juu ya 'meza ya bwana' wameambulia kupigwa faini na mahakama.

Tolu Akintepe, 30, na mke wake Bunmi, 28, walipandishwa kizimbani baada ya kukamatwa wakifanya mapenzi juu ya madhabahu au maarufu kama 'Meza ya bwana' (meza inayokuwa mbele kabisa kanisani).

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Metro, wanandoa hao wakati wakipeana raha juu ya meza ya bwana walifumaniwa na mchungaji wa kanisa hilo dogo la Pentekoste lililopo katika kitongoji cha Ikeja jijini Lagos.

Mchungaji Gbenga Akhiomu aliwataka wanandoa hao walipe fidia ya dola 170 ( takribani Tsh. 225,000) kwa kuivunjia heshima madhabahu.
Mchungaji huyo pia aliwataka wanandoa hao waisafishe madhabahu na kisha wasali kuomba msamaha.

Katika hali iliyowaacha watu wengi mahakamani wakibaki na kicheko, wanandoa hao walimwambia jaji Ifeanyinwa Okenwa kwamba walifanya kitendo hicho ili kuongeza viungo vya kuamsha mapenzi yao ambayo yalikuwa yameanza kufifia baada ya ndoa yao ya miaka minne.

"Mke wangu amekuwa akiniambia mara kwa mara kwamba anataka tuyakuze mapenzi yetu kwa kufanya kitu kisicho cha kawaida" alisema Akintepe.

"Nilifikiria kuwa litakuwa wazo zuri kama tutafanya mapenzi kanisani huku Mungu akituangalia. Nilijua ni wazo linalohitaji ujasiri. Nilimwambia mke wangu naye akalipenda sana".

Jaji Okenwa aliwaonya wanandoa hao waheshimu taasisi za dini na aliwaamuru walipe faini ya dola 170.
Wanandoa hao waliridhika na hukumu hiyo na walijitolea kulisafisha kanisa zima kwa muda wa wiki moja

1 comment:

  1. HIYO NI LAANA NI VILE SIKU HIZI UPAKO HAKUNA WANADAMU TUMEKWENDA MBALI NA MUNGU ZAMANI ADHABU ILIKUWA HAICHELEWESHI SIDHANI WANGEKUWA HAI MUNGU ANGEWASHUGHULIKIA HATA HIVYO NINAKUWA NAWASIWASI IWAPO HILO NI KANISA KAMILI LA PENTOKOSTE

    ReplyDelete